Idara hii inashirikiana na wadau mbalimbali na ina nia ya kutoa huduma ya maji safi na salama kwa ajili ya kunywa kwa kutumia viwango vya Taifa ambavyo ni 400m radius. Mpaka Desemba 2008 Idara ilikuwa imeweza kutoa huduma ya maji katika vijiji 123 kati ya vijiji 207.
Utoaji wa huduma ya maji ulikuwa kama ifuatavyo:-
- Vijiji 12 vilipata maji 100%
- Vijiji 50 vinapata maji kati ya asilimia 50 – 100%
- Vijiji 50 vinapata maji chini ya 50%
- Vijiji 67 vinapata maji chini ya 50%
- Vijiji 77 havina huduma ya maji safi na salama kwa kunywa.
Kutoka na mgawanyo hapo juu ni asilimia 49% tu ya watu waishio Mjini na vijijini ndio wana uhakika wa kupata maji safi na salama kwa ajili ya kunywa, kwa upande wa Mbinga Mjini kiasi cha asilimia 52% tu ndicho hupata maji safi na salama kwa ajili ya kunywa. Teknolojia iliyotumika katika usambazaji wa maji ni:-
- Kutumia pampu zinazoendeshwa kwa generate – mafuta
- Kutumia mwelekeo wa maporomoko (using gravity)
- Kutumia pampu za mkono
- Kutumia (traditional wells)
Mifuko ya Maji (Water Funds):
Kiasi cha asilimia 22.8 ya vijiji 207 vina mifuko ya maji. Lakini hawana kiasi cha kutosha katika mifuko yake kuwezesha kukidhi mahitaji, pia asilimia 65.2 ya miradi ya maji ina kamati za maji, ambazo lakini hazifanyi kazi ilivyotarajiwa, Idara ina watumishi 37 tu kati ya 48 wanaotakiwa na hivyo kuwa na upungufu wa watumishi 11.
Soma zaid kuhusu sekta ya maji hapa |