February 23 2012 4:52:am United Republic of Tanzania-Prime Ministers Office
Quick Links
 
Idara ya Sheria

Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga kama zilivyo Halmashauri nyingine hapa nchini Tanzania inaundwa na Idara na vitengo vyake kadhaa.  Moja ya vitengo hivyo ni kitengo cha Sheria na Usalama kitengo hiki kipo moja kwa moja chini ya Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri (DED).

MUUNDO WA MAJUKUMU YA KITENGO CHA SHERIA KATIKA HALMASHAURI.
Kazi na majukumu ya Halmashauri yameainishwa kwenye katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara za 145 na 167 ya mwaka 1977 na zile sheria za Seikali za mitaaa (Mamlaka za Mamlaka za Wilaya) Sehraia Namba 7 ya 1982.  Wakati katiba inaainisha kuwa kutakuwa na mamlaka/Serikali za mitaa, sheria za Serikali za mitaa Na. 7 ya 1982 zinafafanua majukumu na kazi za Halmashauri ni kama hizi zifuatazo kwa ujumla wake:-

  1. Kudumisha na kuhakikisha kudumisha amani kwenye eneo lake/ eneo la utawala wake.
  2. Kuendeleza uchumi na ustawi wa jamii kwa watu wote katika eneo lake.
  3. Zaidi ya yote kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa kuzingatia sera za Taifa na mipango ya maendeleo vijijini.

Kazi na majukumu makubwa ya Serikali za mitaa ni pamoja na:-

  1. Kutokomeza uhalifu, kudumisha amani na utawala bora.
  2. Kuhimiza, kusimamia na kuimarisha kilimo, biashara na viwanda kueneleza, kuhamasisha na kuimarisha matumizi ya vitendea kazi ili kupambana na umaskini, ujinga na maradhi.

Kwa nyongeza ya majukumu na kazi kama zilivyoainishwa na sheria, sheria hiyo hiyo inaelezea malengo na madhumuni ya Halmashauri kuwa ni kutekeleza kazi na majukumu yaliyoainishwa hapo juu.
Malengo na madhumuni hayo ni pamoja na:-

    • Kutoa/kueleza maana halisi ya mgawanyo wa madaraka/utawala katika siasa, fedha/uchumi na maswala ya uongozi/utawala.
    • Kuendeleza na kusimamia ushiriki wa kidemockrasia na kusimamia maamuzi yanayofanywa na watu wake katika eneo husika.
    • Kuanzisha, kuendeleza na kuimarisha vyanzo mbalimbali vya mapato vya uhakika.
    • Kutoa huduma kwa kiwango cha juu kwa watu wake kwa kushirikiana na vikundi vya kiraia na kujitolea watu binafsi na mamlaka mbalimbali.
    • Kuhamasisha, kuendeleza uelewa na mambo ya mahusiano ya kijinsia kwa watu wake.
    • Kulinda na kusimamia matumizi bora ya mazingira kwa ustawi wa maendeleo bora ya maisha yao.
:.Departments
Afya
Biashara na Masoko
Elimu
Jinsia na Watoto
Maji
Kilimo na Mifugo
Maliasili
Mipango
Majengo na Barabara
Ramani na Ardhi
Sheria
Ushirika
 
.:News!
No New NEWS curently:
Useful Website
Tanzania Government
Prime Minister Office
Tanzania Parliament
Ministry of Finance